Pata taarifa za Ahadi za Wagombea wa Vyama vya Siasa katika Uchaguzi Tanzania.

Ahadi Zangu Screenshot
Ahadi Zangu Screenshot
Ahadi Zangu Screenshot
Ahadi Zangu Screenshot
Update
Mar 27, 2023
Developer
Category
Installs
100+
Rate
0
AhadiZangu ni huduma ambayo imebuniwa na inasimamiwa na GALACHA Co. Ltd, inampa mwananchi taarifa za Ahadi na Ilani za Wagombea na Vyama vya Siasa katika Chaguzi mbalimbali Tanzania. Huduma hii inapatikana kwa kutumia tovuti (AhadiZangu.co.tz).

Awamu ya kwanza ya AhadiZangu hii itakuwa na Wagombea wote pamoja na Ahadi za wagombea na Ilani za Vyama kwa upande wa kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Ahadi zote zinazowekwa katika tovuti zinapatikana Kupitia vyombo vya Habari na Viongozi wa Kampeni wa Mgombea husika, na Ilani tunatumia kutoka kwa vyama husika baada ya Kutolewa hadharani.

Pia Sekta husika zote zitawekwa katika AhadiZangu hii, kuwapa wananchi mwangaza wa kujua sekta husika ina Ahadi na Ilani gani ambayo mgombea ameitaja, na pindi uchaguzi ukishamalizika mgombea teule atawekewa ripoti yake ya kile ambacho amekifanya.

Kwa kupitia AhadiZangu, unaweza kwa urahisi kujua Wagombea au Chama kinasimama wapi katika masuala mbalimbali yahusuyo nchi yetu kwa ujumla.

Chagua Mgombea au Sekta na usome ahadi zote zilizotolewa kwa kipindi chote cha kampeni.
Huduma hii haina uhusiano na Taasisi yoyote au Chama Chochote cha Siasa.