Songs of Salvation
kilichotolewa kwa mara ya kwanza nchini Zaire (kwa
sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC), mwaka
1937. Tangu hapo kimetolewa kwa wingi na hiyo
inathibitisha ya kuwa kimewapendeza wengi.
Toleo jipya limekuwa hitaji kubwa kwa muda mrefu
kwa ajili ya ustawi wa lugha ya Kiswahili, na ni
matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitaleta baraka.
Nyimbo ambazo hazikuandikwa katika kitabu hiki,
zimeachwa ili kutoa nafasi kwa nyimbo nyingine
zitakazoweza kuimbwa kwa urahisi.
Palipo na apostrofi (’) katika maandishi, ieleweke
kwamba silabi moja au herufi moja imeondoshwa kwa
ajili ya mwendo wa sauti ya wimbo, kwa mfano:
’aminiye = aaminiye.’ Ikiwa mstari umewekwa chini ya
neno, ieleweke kwamba badala ya kutamkwa silabi mbili
itamkwe silabi moja tu, kwa mfano: aaminiye au
msalaba.